1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani atembelea Gaza

Sudi Mnette
2 Mei 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametembelea eneo la mpakani la kivuko cha Gaza na kujionea shehena za misaada, baada ya kuitaka Israel kufanya juhudi katika usaidiaji wa eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4fP9R
Tel Aviv Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken akizungumza na jamaa mateka
Tel Aviv Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken akizungumza na jamaa wa mateka - 01/05/2024 Picha: Oded Balilty/AP/picture alliance

Blinken alisafiri hadi Kerem Shalom, eneo la kuingilia Israel katika Gaza kilomita chache kutoka mji wa kusini wa Rafah, ambako aliona malori kadhaa yakisubiri kuingia ikiwa ni pamoja na vifaru kadhaa vya kijeshi vya Israel vikiwa vimeegeshwa pembezoni.

Akiwa kwenye kivuko hicho, Blinken alitembelea karibu na malori 10 katika wakati wa zoezi la kukaguliwa na wanajeshi wa Israel.

Awali Blinken, ambaye katika eneo hilo alisindikizwa na Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alionesha wasiwasi kuhusu kiwango cha misaada inayoingia katika ardhi ya Palestina wakati wa mkutano wake mjini Jerusalem na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.