1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Hamas kufanya tena ziara mjini Cairo

2 Mei 2024

Ujumbe wa kundi la Hamas unatarajiwa hivi karibuni kufanya ziara nchini Misri ili kuendeleza mazungumzo katika dhamira ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4fRPC
Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh
Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh Picha: Fazil Abd Erahim/AA/picture alliance

Nchi wapatanishi katika mzozo huu ambazo ni Marekani, Misri na Qatar zimetoa wito kwa pande zote kuafiki mkataba huo.

Taarifa hiyo iliyotolewa hivi leo imeongeza kuwa Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh amedhihirisha "nia njema" katika kutathmini pendekezo la hivi karibuni la Israel ambalo litajumuisha usitishwaji mapigano kwa siku 40 na kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina.

Soma pia:Blinken aiambia Israel iepuke 'madhara zaidi kwa raia' Gaza

Hata hivyo kumekuwa na hofu kwamba Israel haitokubali kuachana na mpango wake wa kuishambulia Rafah katika dhamira ya kulitokomeza kabisa kundi la Hamas kama alivyosisitiza mara kadhaa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu.