1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiNigeria

Nigeria yaongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali

Amina Mjahid
1 Mei 2024

Kamisheni inayoshughulika na msuala ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali nchini Nigeria imesema nchi hiyo imeongeza mishahara ya wafanyakazi hao kwa kati ya asilimia 25 na 35.

https://p.dw.com/p/4fOdb
Abuja Mji Mkuu wa Nigeria
Abuja Mji Mkuu wa NigeriaPicha: Ute Grabowsky/photothek/picture alliance

Hayo yamejiri wakati taifa hilo lililo na idadi kubwa ya watu na uchumi barani Afrika likikumbana na mgogoro mkubwa wa kupanda kwa gharama ya maisha kwa takriban miongo mitatu.

Mshahara wa chini kabisa wa mfanyakazi wa serikali utakuwa naira 450,000 kwa pesa za Nigeria ikiwa ni sawa na dola 323.97 kwa mwaka, ilisema kamisheni hiyo katika taarifa yake.

Ongezeko hilo la mshahara linawahusisha wafanyakazi wote wa serikali ikiwemo wale walioko katika sekta ya afya, elimu na usalama. Kwa sasa serikali inaendelea na mazungumzo na vyama vya wafanyakazi kufikia makubaliano tofauti ya kiwango cha kitaifa cha mshahara kilichoangaziwa mwisho, mwaka 2019.