SiasaAsia
Bunge la Vietnam laidhinisha uamuzi wa Spika kujiuzulu
2 Mei 2024Matangazo
Hatua ya kuondoka kwa Hue ambayo ilitangazwa tangu wiki iliyopita na Kamati kuu ya Chama, inaiacha Vietnam katika ombwe la uongozi baada ya rais Vo Van Thuong kujiuzulu mwezi Machi, na hivyo kuacha nafasi mbili za juu kati nne bila uongozi.
Soma pia:Ziara ya Xi Vietnam kunatishia usahwishi wa Marekani?
Mnamo Mei 20, Bunge la Vietnam limepanga kuanza mkutano utakaodumu kwa mwezi mzima na ambao unatarajiwa kumteua rais na Spika mpya wa bunge baada ya watu hao kuteuliwa na chama cha Kikomunisti.